• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

TAKUKURU Ruvuma yabaini mapungufu miradi minne ya bilioni 1.5

Imewekwa kuanzia tarehe: March 14th, 2024

Na Albano Midelo

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana ya Rushwa (TAKUKURU) Mkoani Ruvuma imebaini  mapungufu na kuchukua hatua katika miradi minne ya maendeleo yenye thamani ya bilioni 1.55.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma Hamza Mwenda wakati anatoa taarifa ya utekelezaji wa majukumu yake kwa kipindi cha miezi mitatu kwa wanahabari kwenye ukumbi wa Taasisi hiyo uliopo Mahenge mjini Songea.

Mwenda ameitaja miradi iliyobainika kuwa na mapungufu kuwa ni  ujenzi wa madarasa katika shule za msingi Kipapa,Kipika na Mpepai katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga ambapo  kila shule mradi uligharimu  Zaidi ya shilingi milioni 331.

Amesema katika miradi ya shule hizo tatu kulikuwa na changamoto ya mabati kutokuwa na ubora ambapo TAKUKURU iliishauri Kamati za Ujenzi kuyaondoa mabati hayo na kubadilishwa na tayari  Kamati zilitekeleza kwa kuweka mabati yenye ubora.

Mwenda ameutaja mradi mwingine uliobainika  kuwa na mapungufu ni ujenzi wa sekondari mpya Kijiji cha Lugagara  Kata ya Kilagano Halmashauri ya Wilaya ya Songea ambapo serikali ilitoa Zaidi ya shilingi milioni 560 kutekeleza mradi huo.

“Hata hivyo kwenye mradi huu kulikuwa na changamoto ya baadhi ya mafundi walioingia mkataba na mwajiri kutokuwepo eneo la mradi hivyo kusababisha mradi kuwa nyuma ya muda’’,alisema Mwenda.

Amesisitiza kuwa TAKUKURU ilimshauri Mhandisi kuwafuatilia mafundi hao na kuhakikisha wanakuwepo eneo la mradi ili uweze kukamilika kwa wakati.

Mkuu huyo wa TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma amesema katika kipindi hicho  waliweza  kufuatilia miradi 23 ya maendeleo yenye thamani ya Zaidi ya shilingi bilioni 4.66 ambapo ufuatiliaji huo umefanyika katika miradi ya ujenzi wa madarasa katika shule mpya saba za sekondari na  ujenzi wa nyumba mbili za walimu.

Ameongeza kuwa TAKUKURU katika kipindi hicho imefanya kazi moja ya uchambuzi wa mfumo uliohusu mfumo wa utoaji huduma za sekta ya ardhi katika Wilaya ya Songea,Tunduru na Namtumbo lengo likiwa ni kuangalia uzingatiaji wa sheria,kanuni na miongozo.

Amesema katika uchambuzi huo mambo mbalimbali yalibainika na kuchukuliwa hatua ambapo ameyataja mapungufu hayo kuwa ni ukosefu wa upatikanaji wa usafiri wa uhakika,uhaba wa wafanyakazi na  maafisa Ardhi na watoa huduma kutotambua vema mkataba wa kisheria wa utoaji huduma.

Mwenda amesema katika kipindi hicho cha miezi mitatu TAKUKURU wameweza kupokea jumla ya malalamiko 55 ambayo yameshughulikiwa kwa mujibu wa sheria kwa kuanzisha uchunguzi ambao upo  katika hatua mbalimbali.

Ameyataja matarajio ya kipindi cha miezi mitatu ijayo kuwa ni kuendelea kuelimisha  wananchi juu ya rushwa na madhara yake,lengo likiwa ni kuwawezesha wananchi kupata uelewa kuhusu rushwa .

Ametoa wito kwa wananchi mkoani Ruvuma kuendelea kuunga mkono jitihada za kufichua vitendo vya rushwa na walarushwa kwa kutoa taarifa sahihi zitakazowezesha kuwachukulia hatua wahusika.

Baadhi ya wanahabari mkoani Ruvuma wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa TAKUKURU Mkoani Ruvuma Hamza Mwenda 

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.