• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

TFS MADABA ilivyodhamiria kudhibiti uchomaji moto misitu

Imewekwa kuanzia tarehe: November 12th, 2022

SERIKALI imewataka wadau wa misitu katika Halmashauri ya Madaba mkoani Ruvuma,kuunganisha nguvu zao katika kukabiliana na uharibifu wa misitu ili kuwa na misitu endelevu kwa ajili ya kuharakisha maendeleo na ukuaji wa uchumi nchini.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa wilaya ya Songea Pololet Mgema,wakati akifungua mkutano wa wadau wa misitu na wenye mashamba ya miti jirani na shamba la miti Wino ulioandaliwa na wakala wa huduma za misitu Tanzania(TFS).

Alisema,pamoja na jitihada mbalimbali zinazofanywa na serikali kupitia shamba la miti Wino katika kusaidia kupambana na matukio ya matukio ya moto yanayotokea kwenye mashamba ya miti na misitu ya asili,lakini bado kuna kiwango kikubwa cha uchomaji moto na uharibifu wa mazingira.

Mkuu wa wilaya alisema,uharibifu huo usipodhibitiwa haraka serikali na wadau  watalazimika kuingia gharama kubwa ya kurejesha hali nzuri ya mazingira na kusababisha hata kizazi  kijacho kushindwa kunufaika na rasilimali za misitu zilizopo katika Halmashauri hiyo.

Mgema alitoa mfano,mwaka 2021  pekee jumla ya ekta 1,663 za miti  katika shamba la Wino zilichomwa moto na watu wasiofahamika na kuitaka jamii inayoishi kuzunguka shamba hilo kuwa walinzi kwani lina mchango mkubwa kiuchumi kwa Halmashauri,mkoa na Taifa.

Amewataka wataalam wa misitu kushirikiana na viongozi wa serikali za vijiji na kata kutoa elimu kwa jamii ya kuanza kutumia nishati mbadala ikiwamo gesi  ili kuepusha Halmashauri hiyo kugeuka jangwa kutokana na matumizi makubwa ya kuni na mkaa yanayofanywa na wananchi.

Katika hatua nyingine Mgema,ameitaka wakala wa huduma za misitu Tanzania(TFS) kupitia shamba la miti Wino kuongeza vifaa vya kuzimia moto ili viweze kutumika pindi moto unapotokea kwenye mashamba  ya miti ya kupandwa na asili.

Aidha ameagiza,kuanzia mwezi Januari mwakani  kila kaya iwe na  shamba la miti  kuanzia nusu eka na watu wote wenye umri wa miaka 18 na kuendelea kuhakikisha kila mmoja anapanda miti 5 kuzunguka eneo analoishi.

Kwa upande wake Mhifadhi Mkuu wa shamba la miti Wino Glory Kasmir alisema, TFS kupitia shamba la Wino imejipanga kuongeza kasi ya upandaji miti kutoka ekta 500 za sasa hadi kufikia ekta 3,000 katika maeneo ya Mkongotema na Ifinga Halmashauri ya Madaba wilayani Songea.

Kasmir alieleza kuwa,malengo ya kuanzishwa kwa hifadhi ya msitu wa Wino ni kuhifadhi maliasili zinazotaka kutoweka ikiwamo vyanzo vya maji,kuzalisha mbao,nguzo za umeme kwa siku za usoni na kutoa ajira kwa wananchi  hasa wale wanaotoka katika vijiji jirani.

Amewapongeza wadau wanaojihusisha na upandaji miti,kutokana na mchango mkubwa katika utunzaji mazingira  ambapo ameshauri baada ya upandaji wa miti wahakikishe wanahudumia miti hiyo kwa kufanya usafi wa mashamba yao ,kufanya doria na kufungua barabara za ndani na nje ya mashamba.

Mmoja wa wadau wa misitu Dkt  Arnold Wella, ameishauri Serikali kupitia wizara ya maliasili na utalii kuanzisha kikosi maalum cha askari ambao kazi yao ni kuzuia matukio ya moto kwenye mashamba ya miti ya kupandwa na misitu ya asili.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • KIONGOZI mwenge wa Uhuru aonya rushwa kwenye uchaguzi

    May 10, 2025
  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.