Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea mkoani Ruuvma wameipongeza Serikali kwa huduma bora ya matibabu wanayoipata katika Hospitali ya Wiliya ya Songea iliyopo kata ya Mpitimbi.
Wananchi hao wametoa pongezi hizo kwenye ziara iliyofanywa na Mkurugenzi wa Mtandao wa Utawala Bora Mkoa wa Ruvuma Michael Sadic katika Hospitali hiyo.
Wakizungumza na vyombo vya habari wameishukuru serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Mhe Rais wa Awamu ya Sita Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuona umuhimu wa watu wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea kujengewa hospitali na kupata huduma bora za afya .
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.