Wananchi wa Kata ya Mkongotema, Halmashauri ya Madaba wilayani Songea mkoani Ruvuma wameelezea furaha yao kuhusu utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Jimbo la Madaba.
Wakizungumza katika mkutano wa Mbunge wa Jimbo la Madaba Dkt Joseph Mhagama Wamekiri kuwa miradi ya maendeleo iliyotekelezwa imeondoa changamoto nyingi zilizowakabili, huku wakifurahia kuboreshwa kwa huduma muhimu kama maji, umeme, elimu, na afya.
Hazidu Mussa Njozi, mkazi wa Kijiji cha Lutukila, amesema kero zilizokuwepo zimepatiwa ufumbuzi na kusisitiza kuwa Mbunge Mhagama ameonesha dhamira ya dhati kwa wananchi.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Ndelenyuma, Stanley Ngairo, amepongeza juhudi za mbunge huyo na kusema miradi ya maendeleo inayoendelea katika maeneo yao imeleta mabadiliko makubwa.
Katika ziara yake ya kikazi, Mbunge Joseph Mhagama alieleza kuwa lengo la Serikali ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za kijamii.
Amesema sasa wakazi wa Mkongotema wanapata huduma muhimu kama maji, umeme, barabara, afya, na elimu, ambazo awali zilikuwa changamoto kubwa kwao.
Mhagama ameongeza kuwa mradi wa kusambaza maji kutoka Lutukila hadi Mtazamo umetekelezwa na kusaidia wakazi waliokuwa na changamoto ya maji safi.
Kata hiyo inatarajia kupokea Shilingi bilioni 1.12 kwa ajili ya ujenzi wa shule ya sekondari, huku umeme ukiwa umesambazwa hadi maeneo ya mbali ambayo awali hayakuwa na huduma hiyo muhimu.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.