Watoto watatu wamefariki dunia na wengine wanne wamelazwa katika Kituo cha Afya Lusewa baada ya kupigwa na radi katika Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo.
Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo, Mheshimiwa Ngollo Malenya, amewatembelea waathirika wa tukio hilo, akiwafariji majeruhi na kutoa mkono wa pole kwa familia za wafiwa kutoka vitongoji vya Mchangila, Ligunga, na Zanzibar.
Kwa mujibu wa taarifa, tukio hilo limeathiri zaidi familia moja ambayo imepoteza watoto wawili, huku mtoto mmoja akitoka familia nyingine.
Akizungumza baada ya ziara hiyo, Mheshimiwa Malenya amewataka wananchi kuwa waangalifu nyakati za mvua, akiwahimiza kuepuka kukaa karibu na miti ili kuepuka madhara ya radi. Pia amesisitiza mshikamano wa jamii katika kusaidiana na kuwafariji waliopata msiba huo mzito.
Tukio hili linajiri wakati mvua kubwa zikiendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali ya nchi, na mamlaka zinahimiza tahadhari zaidi dhidi ya majanga ya asili.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.