Mkaguzi Mkuu wa Nje kutoka Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi CPA Deogratias Waijaha amesema watumishi wapya 675 kutoka Halmashauri za wilaya ya Mbinga,Nyasa na Mbinga mji mkoani Ruvuma hawajafanyiwa upekuzi ili wakae sawa kwenye utumishi wa umma.
CPA Waijaha amesema hayo wakati anazungumza kwa nyakati tofauti katika kikao maalum cha Baraza la madiwani cha kujadili taarifa ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) juu ya hoja na mapendekezo CAG kwa hesabu za Mamlaka ya Serikali za Mitaa kwa mwaka wa fedha wa 2022/2023 katika Halmashauri hizo.
Mkaguzi Mkuu huyo amebainisha kuwa kati ya watumishi hao watumishi 369 wameajiriwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga,watumishi 225, Halmashauri ya Nyasa na watumishi 81 wa Halmashauri ya Mji Mbinga ambapo ameagiza watumishi hao kufanyiwa upekuzi ili wakidhi sifa ya utumishi wa umma.
Hata hivyo Halmashauri zote nane za Mkoa wa Ruvuma zimepata Hati Safi katika ukaguzi wa CAG uliofanywa katika mwaka 2022/2023.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.