Mkuu wa Wilaya ya Songea Mheshimiwa Kapenjama Ndile akizungumza kwenye maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari Duniani kimkoa zilizofanyika kwenye ukumbi wa Manispaa ya Songea ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahmed Abbas Ahmed
Akizungumza kwenye maadhimisho hayo Mkuu wa Wilaya ya Songea Mheshimiwa Kapenjama Ndile amesema katika Tanzania sheria zinawapa heshima kubwa waandishi wa Habari na kwamba Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazoheshimu uhuru wa Habari.
Ndile amesisitiza kuwa huwezi kuheshimu vyombo vya Habari bila kuheshimu wanahabari wenyewe ambapo amesema wanahabari wamefanyakazi kubwa iliyotuka katika wilaya ya Songea na Mkoa wa Ruvuma kwa ujumla.
Naye Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Ruvuma Amon Mtega amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma kwa kuyaunganisha makundi mbalimbali wakiwemo wanahabari .
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.