ASKARI 20 wa Uhifadhi wa vijiji (VGS) wamesaini mkataba wa kufanya kazi ya ulinzi wa maeneo ya Jumuiya za wanayamapori za Chingoli na Nalika wilayani Tunduru mkoani Ruvuma.
Mkuu wa Wilaya ya Tunduru,Mhe. Simon Chacha ameshuhudia zoezi la utiaji wa saini kwa Askari hao wa Uhifadhi
Akizungumza kwenye hafla hiyo Mkuu wa Wilaya amesisitiza kuwa Juhudi zinazofanywa na serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa Uhifadhi wa kuwapatia mafunzo Askari ambao watakuwepo maeneo ya vijiji, ili kuhakikisha inaondoa migongano kati ya Binadamu na Wanyama.
Mpaka sasa Wilaya ya Tunduru ina jumla ya Askari wa Uhifadhi wa Kijiji (VGS) 210.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.