• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

ASKARI wanyamapori 106 wahitimu mafunzo maalum ya uhifadhi Namtumbo

Imewekwa kuanzia tarehe: June 16th, 2021

JUMLA ya askari 106 kati 110 wa wanyamapori wa vijiji (VGS) kutoka jumuiya za wanyamapori nchini, wamehitimu mafunzo ya kozi maalum katika chuo cha mafunzo ya uhifadhi wa maliasili kwa jamii Likuyu Sekamaganga wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma.

Mkuu wa chuo hicho Jane Nyau amesema,mafunzo hayo ni mkakati wa Serikali kupitia wizara ya maliasili na utalii kuwajengea uwezo na kuwapa mbinu askari hao wa vijiji kukabiliana na wanyamapori wakali na waharibifu kwa jamii zinazoishi kando kando ya maeneo yaliyohifadhiwa.

Nyau alitaja jumuiya wanazotoka wanafunzi hao hao ni hifadhi ya msitu wa Engoserosambu wilaya ya Ngorongoro ni 6 , na 100 wanatoka jumuiya za Mbarang’andu,Kimbanda na Kisungule zilizopo wilaya ya Namtumbo na jumuiya ya Nalika na Chingolo iliyopo katika wilaya ya Tunduru kwa ufadhili wa Shirika la Word Wide Fund For Nature (WWF).

Hata hivyo amesema, wanafunzi wanne waligomea mafunzo na kuondoka chuoni ambao ni Jafari Abdala,Mohamed Mchamedi wa jumuiya ya Chingoli,Swalehe Mbalale wa jumuiya ya Nalika na Milkion Ponera wa jumuiya ya Kimbanda.

Amesema, chuo hicho ni mojawapo ya vyuo vya Serikali chini ya Wizara ya maliasili na utali chenye wajibu wa kutekeleza mkakati huo kwa kuijengea jamii uwezo kwa njia ya mafunzo ili iweze kukabiliana na wanyamapori wakali na waharibifu kwa lengo la kupunguza migogoro kati ya binadamu na wanyamapori.

Mkuu huyo wa chuo amesema, ni ukweli usiopingika kuwa,kwa sasa idadi ya watu nchini imeongezeka na ongezeko hilo linakwenda sambamba na shughuli za kibinadamu kama kilimo,ufugaji na nyinginezo hali inayopelekea mwingiliano kati ya shughuli za binadamu na rasilimali za maliasili.

Alibainisha kuwa, kuongezeka kwa shughuli za kibinadamu kumepelekea kukithiri kwa uharibifu wa mazingira ikiwemo ukataji miti,kuziba kwa shoroba, maeneo mtawanyiko wa wanyamapori, uharibifu wa vyanzo vya maji na athari nyingine.

Amesema, matumaini ya serikali chini ya wizara ya maliasili na utalii wahitimu hao watakuwa mabalozi na walimu wazuri kwa jamii na kupeleka elimu hiyo kwa wananchi wa maeneo yao ili nao waweze kunufaika.

Aidha,amewashauri wananchi hasa wanaoishi kando kando ya maeneo ya hifadhi, kuanza kulima mazao ambayo hayapendwi kuliwa na wanyamapori kama Tembo,ikiwemo ufuta,alizeti na kupanda pilipili kuzunguka mashamba yao kama njia mbadala ya kuepuka kuvamiwa na wanyama hao katika maeneo yao.

Kwa upande wake mwakilishi wa Mkuu wa wilaya ya Namtumbo Alkwin Ndimbo amewaasa wahitimu hao kutambua kwamba, kazi ya uhifadhi inahitaji uzalendo,uadilifu na uaminifu katika ulinzi wa rasilimali za nchi yetu.

Hivyo amewataka kwenda kusimamia vyema tunu na rasilimali za nchi, na kujiepush na tamaa wakati wote wa majukumu yao ya ulinzi ili kuleta tija kwa jamii na nchi kwa jumla.

Amesisitiza, suala la uzalendo na uvumilifu kwani ndiyo sehemu wajibu katika kazi za kila siku na ni sehemu ya kiapo chao tofauti na watumishi wengine wa umma.

Amewaasa kwenda kufanya kazi kwa weledi na kuzingatia sheria za uhifadhi na kuonyesha nidhamu ya hali ya juu kwa jamii inayowazunguka badala ya kutumia mafunzo waliyopata kunyanyasa wananchi wengine hasa pale zinapofanyika operesheni za kuwaondoa wavamizi kwenye misitu na rasilimali mbalimbali.

Akisoma risala kwa niaba ya wahitimu Masoud Nyoni amesema, katika mafunzo hayo wamepata elimu stahiki juu ya uhifadhi na matumizi ya endelevu ya maliasili vijijini kwa maendeleo endelevu.

Amesema,elimu hiyo imegusa nyanja mbalimbali za uhifadhi wa maliasili kupitia masomo tofauti kama sheria za uhifadhi,utambuzi wa wanyamapori na matumizi ya silaha hifadhini.

Kwa mujibu wa Nyoni,mafunzo mengine ni matumizi ya GPS na ramani,huduma ya kwanza,maadili katika uhifadhi, ukakamavu, haki za binadamu,mbinu za doria, intelejensia, upelelezi,upekuzi na ukamataji majangili.

Ameiomba Serikali kuboresha mazingira ya mafunzo kwa wanafunzi wa chuo kama upungufu wa mabweni,vitendea kazi kama silaha,fedha,mahema,GPS,radio call, na viona mbali.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.