Wizara ya Maliasili na Utalii inamatarajio makubwa ya kuimarika kwa shughuli za doria za kudhibiti wanyamapori wakali na waharibifu na hivyo kupunguza migongano baina ya binadamu na wanyamapori baada ya wahitimu zaidi ya kuhitimu fanyi ya uwaskari wa Wanyamapori.
Hayo yamesemwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Kamisha wa Polisi (CP) Benedict Wakulyamba alipokuwa akifunga mafunzo maalum kwa Askari Wahifadhi toka TAWA na kozi Na. 73/2024 kwa Askari Wanyamapori wa Vijiji (VGS) katika Chuo cha Likuyu Sekamaganga Wilaya ya Namtumbo Mkoa wa Ruvuma.
CP Wakulyamba ametaja matarajio mengine ya Wizara kwa wahitimu hao ni Pamoja na kuongezeka kwa ufanisi wa kuitikia kwa haraka kwenye matukio kutokana na kuwa, VGS mnaohitimu mtakuwa kwenye maeneo yenye changamoto na hivyo kuwa mstari wa mbele katika kudhibiti wanyamapori wakali na waharibifu kabla hawajasababisha Mathara.
Aidha CP. Wakulyamba ametoa wito kwa wananchi kuzingatia maelekezo yanayaotolewa na wataalamu wa taasisi za uhifadhi ili kuepuka madhara ya wanyamapori wakali na waharibifu, kuzingatia mpango wa matumizi bora ya ardhi katika maeneo yaliyopo jirani na hifadhi, mapito na mtawanyiko wa wanyamapori na kujiepusha na tabia ya kupiga wanyamapori wakali kwa kutumia silaha mbalimbali za kimila/jadi pindi wanapoingia kwenye maeneo ya wananchini.
Akimkaribisha mgeni rasmi, Mkuu wa cha Uhifadhi wa Vijiji kwa Jamii Likuyu Sekamaganga, Bi Jane Nyau ameeleza jumla ya Askari Wahifadhi ishirini na nane (28) toka kwenye Mapori ya Akiba ya Selous na Liparamba na VGS mia moja ishirini na mbili (122) kutoka Wilaya thelathini na nne (34) wamehudhuria mafunzo haya.
Naye Mkurugenzi wa Kitengo cha Utafiti na Mafunzo Dkt. Edward Kohi amesema Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia vyuo vyake vya mafunzo itaendelea kutoa Mafunzo mbalimbali ya Uhifadhi kwa kuwajengea uwezo Askari wa Jeshi la Uhifadhi pamoja na Askari wa Wanyamapori wa Vijiji ili kuimarisha Shughuli za Uhifadhi kwa kushirikiana na wanavijiji waishio jirani na Hifadhi.
Msimamizi Mkuu wa Mradi wa Frankfurt Zoological Society Bi. Kathryn Doody licha ya kuipongeza Serikali kwa kuendesha Mafunzo kwa askari wa Jeshi la Uhifadhi na VGS, amewakumbusha askari hao kutambua kuwa kazi wanayofanya ni muhimu sana, siyo kwa Tanzania tu bali kwa ulimwengu wote.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.