MRADI wa Barabara ya Mbinga Mbambabay yenye urefu wa kilomita 66 umekamilika kwa asilimia 100 na kugharimu kiasi cha shilingi bilioni 129.
Akizungumza Mhandisi wa Wakala wa Barabara Tanrod Justin Mlope Mkoa wa Ruvuma amesema mradi huo umefanyika kwa mda wa miezi 33 kuanzia Aprili 3,2018 hadi Januari 2,2021 na kukamilika kwa wakati.
Mrope amesema kupitia mradi huo mara baada ya kukamilika kipindi cha matazamio kilianza Januari 2,2021 na hadi kufikia sasa kimeisha na barabara imeanza kutumika.
“Gharama za mradi ilikuwa shilingi bilioni 129 kupitia ufadhili wa Benki ya maendele ya Afrika na Mfuko wa Maendeleo wa Afrika “.
Amesema mradi huo umejumuisha na ujenzi wa sehemu maegesho ya maroli katika Wilaya ya Nyasa katika Bandari ya Mbambabay kwaajili ya kubeba mizigo na kupeleka Bandari ya Mtwara.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Kitengo cha Habari Serikalini Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma
Juni 1,2022
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.