BARAZA la madiwani katika Halmashauri ya wilayanya Songea mkoani Ruvuma limetoa rai kwa watalaamu wa Halmashauri hiyo kuongeza jitihada zaukusanyaji wa mapato ili kuongeza mapato ya ndani.
Akizungumza kwenye kikao hicho,Kaimu Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Mheshimiwa Simon Kapinga ambae ni Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri amewataka wataalamu kuendelea na zoezi la doria katika ukusanyaji wa mapato ili kuongeza mapato ambayo yatakwenda kukamilisha miradi iliyopo katika Kata na Vijiji na shughuli za maendeleo.
WAHESHIMIWA Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea wamefanya Baraza la robo ya nne kwa mwaka ulioishia Juni 2023 leo tarehe 24/08/2023 katika ukumbi wa mikutano Lundusi-Peramiho.
Baraza hilo limeudhuriwa na Waheshimiwa Madiwani, Mkurugenzi Mtendaji, Wakuu wa Idara na Vitengo, Watendaji wa Kata, Wataalamu kutoka TAKUKURU, Usalama na Ofisi ya RAS.
Sambamba na hilo Mhe. Kapinga amewataka Watendaji wa Kata na Vijiji kufanya mikutano ya hadhara yenye lengo la kuwahimiza wananchi kutunza mazao kwa ajili ya chakula.
“Bei ya mazao kwa sasa ipo juu hivyo Watendaji katika mikutano hiyo waambieni wananchi wasidanganyike na bei hizo wakapata tamaa ya kuuza chakula chote wajitahidi kutunza chakula kingine kwa ajili ya familia”, amesisitiza Mhe. Kapinga.
Vilevile Mheshimiwa Kapinga amesisitiza Idara za Elimu Msingi na Sekondari kufanya jitihada za makusudi kwa shule ambazo zina wanafunzi wa jinsia ya kike na kiume ambazo hazina walimu wa kike ziweze kupelekewa kwani itasaidia wanafunzi hao kuwa huru kuelezea changamoto zao.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.