Benki ya Dunia imetoa shilingi milioni 220 kutekeleza Mpango endelevu wa Maji na Usafi wa Mazingira katika Halmashauri ya Wilaya Songea Mkoani Ruvuma.
Kaimu Mganga mkuu wa Halmashauri hiyo Dr Geofrey Kihaule amesema fedha hizo zimetolewa kwa madhumuni ya kutekeleza ujenzi na uboreshaji wa miundo mbinu ya kutolea huduma za afya kwenye Zahanati.
Amesema miundo mbinu inayotakiwa kujengwa na kuboreshwa ni chumba cha kujifungulia akinamama wajawazito, chenye viwango vinavyokubalika Kimataifa,matundu saba ya vyoo ikijuisha choo ya walemavu,kichomea taka,na miundo mbinu ya kutolea huduma ya maji.
Dr kihaule amesema ujenzi wa miundo mbinu ya kutolea huduma za afya kwenye zahanati kutasaidia wananchi hususani akinamama kuwa katika mazingira salama ya kujifungulia na mazingira ya faragha pindi wanapofika katika vituo hivyo.
Dr kihaule amevitaja Vijiji 10 ambavyo vitanufaika na mradi huo kuwa ni Litowa,Parangu,Lugagara,Peramiho (B),Muungano Zomba,Vijiji ni vingine ni Mgazini,Kilagano,Ngahokora,Liula na Kikunja.
Ameongeza kwa kusema muda wa utekelezaji wa mradi ni siku 40 kulingana utaratibu uliopanga wa utekelezaji,katika kufanikisha kazi hiyo vikao kazi baina ya kamati za afya za Vijiji na viongozi wa Serikali za vijiji tayari vimefanyika na ujenzi unatarajia kuanza mara moja kuanzia mwezi Mei 17,2021.
Kwa upande wake Afisa Afya wa Wilaya hiyo na Mratibu wa mradi huo John Kapitingana amesema mradi wa mpango endelevu wa maji na usafi wa mazingira unafadhiri kwa utaratibu wa lipa kulingana na matokeo (EP4R).
“Tushrikiane katika kutoa matokeo chanya ya mradi”,amesisitiza Kapitingana.
Kapitingana ametoa wito kwa viongozi wa vijiji na wananchi kujenga mshikamo na ushirikiano katika kufanikisha ujenzi huo na kutoa matokea chanya ambayo yatasababisha Benki ya Dunia kuendelea kutoa ufadhili kwa zahanati nyingi katika halmashauri.
Baadhi ya viongozi wa kamati ya afya ya Kijiji cha Litowa ambao ni Lukulesi mkinga na abdallah kassimu wamesema wameupokea mradi na watashirikiana na wananchi kuhakikisha mradi huo unakamilika kwa wakati na unatoa huduma iliyokusudiwa.
Halmashauri ya Wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma inajumla ya Zahanati 24,kituo cha Afya kimoja na Hospitali moja ya Wilaya iliyojengwa Kijiji cha Mpitimbi (B) kata ya Mpitimbi.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.