• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

BENKI ya NMB yatoa vifaa vya milioni 15 katika shule tatu Mbinga

Imewekwa kuanzia tarehe: July 6th, 2022

BENKI ya NMB imeweza kutoa msaada wa  madawati na viti  vyenye thamani ya shilingi milioni 15 katika shule tatu wilayani Mbinga mkoani Ruvuma.

Msaada huo umekabidhiwa na NMB kwa Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Peter Ntalamka katika hafla iliyofanyika katika shule ya sekondari Kipapa.

Akizungumza kabla ya kukabidhi msaada huo,Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kusini Janeth Shango amezitaja shule ambazo zimepata msaada huo kuwa ni shule ya msingi Luposo iliyopata madawati 50 yenye thamani ya shilingi milioni tano.

Shule nyingine amezitaja kuwa ni shule ya sekondari Kiamili ambayo imepata msaada wa viti 50 na meza 50 vyenye thamani ya shilingi milioni tano na shule ya sekondari ya Kipapa ambayo imepewa msaada wa viti 50 na meza 50 vyenye thamani ya shilingi milioni tano.

“Vifaa hivi ambavyo tunavikabidhi leo,ni moja ya ushiriki wetu katika maendeleo ya jamii na sisi kama benki  inayoongoza Tanzania,tunaowajibu wa kuhakikisha jamii inayotuzunguka inafaidika kutokana na faida tunayopata’’,alisisitiza Shango.

Hata hivyo Meneja huyo wa Kanda ya Kusini,amesema kwa miaka kadhaa sasa Benki ya NMB imekuwa ikisaidia miradi mbalimbali ya maendeleo kwa wananchi kwa kujikita Zaidi kwenye miradi ya elimu na afya ambako imekuwa inatoa madawati,vifaa vya kuezekea,vitanda na magodoro  yake  Pamoja na kusaidia majanga yanapotokea nchini.

Kwa upande wake mgeni rasmi katika hafla hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Aziza Mangasongo ambaye aliwakilishwa na  Peter Ntalamka ameipongeza NMB kwa kutoa msaada huo kwa shule tatu za Wilaya hiyo ambapo amesema msaada huo utasaidia kuboresha taaluma kwa wanafunzi.

Amesema Benki ya NMB imekuwa kila mwaka inatoa misaada mbalimbali katika shule za Wilaya ya Mbinga ambapo mwaka jana ilisaidia vifaa vya kuezekea  bweni lenye thamani ya shilingi milioni 80 katika shule ya sekondari Litembo.

Naye Mkuu wa shule ya sekondari ya Kiamili Mary Ndunguru akizungumza baada ya kukabidhiwa msaada wa viti na meza kutoka NMB,ameipongeza Benki hiyo kwa kutatua changamoto ambazo zilikuwa zinaikabili shule hiyo.

Amesema shule yake yenye wanafunzi  Zaidi ya 1000,kabla ya NMB kutoa msaada huyo ilikuwa na upungufu wa meza na viti Zaidi ya 300 ambapo hivi sasa changamoto ya wanafunzi wawili kukaa kiti kimoja imepungua,hata hivyo ametoa rai kwa NMB kuendelea kutoa msaada katika shule kwa sababu changamoto bado zipo.

Kwa upande wake Mwanafunzi wa shule ya sekondari Kipapa Flora Komba akizungumza kwa niaba ya wanafunzi wenzake,ameipongeza NMB kwa msaada huo ambao  amesema umepunguza changamoto ya viti na meza kwa wanafunzi.

NMB ndiyo Benki ambayo imezifikia wilaya zote nchini kwa asilimia 100,ikiwa na matawi 226 na ikiwa na idadi ya wateja Zaidi ya milioni nne.

Imeandikwa na Albano Midelo

Mbinga

Julai 5,2022

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.