RAIS Dkt Samia Suluhu Hassan ametoa zaidi ya shilingi bilioni 20 kujenga sekondari mpya 11 na vyumba vya madarasa 656 katika Mkoa wa Ruvuma.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas amesema kati ya fedha hizo zaidi ya shilingi bilioni 10 zilitolewa kupitia UVIKO ambazo zimejenga madarasa 500,shilingi bilioni 7.7 zimejenga shule mpya za sekondari 11 kupitia program ya SEQUIP na shilingi bilioni 3.1 zimejenga madarasa 156 katika shule za sekondari mkoani Ruvuma.
“Serikali imetekeleza wajibu wake kilichobaki ni wajibu wa wazazi kuhakikisha watoto wao wanahudhuria shule “,alisisitiza Kanali Thomas .
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.