Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imetoa zaidi ya shilingi bilioni 22 kwaajili ya ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami katika Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma.
Mkuu wa Wilaya ya Songea, Mhe. Kapenjama Ndile, amesema walipokea fedha hizo mwaka 2024 kwaajili ya ujenzi wa barabara na mpaka hivi sasa mradi huo upo katika hatua za umaliziaji na barabara hizo zimeufanya mji wa Songea kuwa wa kisasa na unaopendeza kwa kuwa mwanzo hapakuwa na barabara nzuri.
Mkazi wa Manispaa ya Songea, Josephina Fred, amesema barabara hizo zimekuja kuwasaidia ukilinganisha na mwanzo ambapo walikuwa wakipata changamoto nyingi hasa kwa wao wafanyabiasha lakini sasa wateja wanafika na usafiri wao na kwa wakati ambapo inawasaidia kufanya biashara.
Kwa upande wake mkazi mwingine wa Manispaa ya Songea, Masumbuko Kayuni, amemshukuru Serikali ya Awamu ya Sita kwa kuwaletea barabara nzuri ambazo sasa zimekuwa zikiwasaidia katika usafiri wa magari, pikipiki na hata watembea kwa miguu.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.