SERIKALI ya Awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan imetoa fedha zaidi ya shilingi bilioni tatu kwaajili ya ujenzi wa Hospitali ya Halmashauri ya Madaba wilaya ya Songea mkoani Ruvuma
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba Idris Mohamed Sajid amesema amesema katika kipindi cha mwaka wa fedha 2022/2023 Halmashauri ilipokea kiasi cha shilingi milioni 834 kwaajili ya ujenzi wa Hospitali hiyo na kufikia hatua ya ukamilishaji.
Hata hivyo amesema katika kwa mwaka wa fedha 2023/2024 Halmashauri hiyo imepokea kiasi cha shilingi Milioni 900 kwaajili ya utekelezaji wa ujenzi wa Hospitali ya Wilaya,ukamilishaji wa Zahanati ya Mahanje,pamoja na Zahanati ya Ifinga.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo utekelezaji ujuenzi wa Zahanati ya Mahanje umekamilika na mradi unatoa huduma kwa wananchi,ukamilishaji wa Zahanati ya Ifinga unaendelea pamoja na Hospitali ya Wilaya.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.