BODI ya Maji Bonde la Ruvuma na Pwani ya Kusini imepokea Pikipiki 10 kutoka Wizara ya Maji na kugawa kwa Jumuiya za watumia Maji.
Akizungumza wakati wa Makabidhiano ya Pikipiki hizo mara baada ya Kikao cha uzinduzi wa Jukwaa la wadau wa usimamizi na uendelezaji wa Rasilimali za Maji kilichofanyika Veta Manispaa ya Songea Mwenyekiti wa Bodi ya Bonde la Ruvuma na Pwani ya Kusini Cosmas Masawe amesema pikipiki hizo kwaajili ya utendaji wa kutembelea vyanzo vya Maji na kuhakikisha vinakuwa salama.
Masawe akimkabidhi pikipiki Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watumia Maji ya Mto Lumeme Kaskazini John Nzuyu amesema kila aliyekabidhiwa kifaa cha usafiri ahakikishe anakitumia na kukitunza vizuri ili yasitokee makosa kwenye vyanzo vya Maji.
Mkurugenzi wa Bodi ya Maji Bonde la Ruvuma na Pwani ya Kusini Sudi Mpemba amesema lengo la kupata pikipiki kutoka Wizara ya Maji ni kuirahisishia Jumuiya za watumia Maji kufuatilia vyanzo vya Maji kwa urahisi na kuhakikisha haviharibiwi na vinakuwa salama kwaajili ya matumizi endelevu.
“Tumefanya jambo kubwa sana kuhakikisha Rasilimali za Maji zinalindwa kwa zoezi ambalo amelifanya Mwenyekiti wetu wa Bodi ya Maji Bonde la Ruvuma na Pwani ya Kusini kugawa kifaa cha utendaji cha usafiri wa kusimamia Rasilimali za Maji “.
Mpemba amesema wamepokea pikipiki kutoka Wizara ya Maji kwaajili ya Jumuiya ya Watumia Maji kwa Mabonde yote,ikiwa Bonde la Ruvuma na Pwani ya kusini imepata pikipiki 10 na saba imegawiwa kwa Jumuiya na 3 zimegawiwa kwa ofisi ndogo za Mabonde zilizopo Lindi,Tunduru na Songea.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Afisa Habari Halmashauri ya Madaba
Desemba 2,2020.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.