Mkuu wa Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma anayemaliza muda wake, Mhe. Simon Chacha, amekabidhi rasmi ofisi kwa Mkuu mpya wa Wilaya hiyo, Mhe. Denis Masanja, katika hafla iliyofanyika Juni 26, 2025 kwenye ofisi za Mkuu wa Wilaya Tunduru.
Tukio hilo lilihudhuriwa na wajumbe wa Kamati ya Usalama ya Wilaya na viongozi mbalimbali wa Serikali.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mhe. Chacha alitoa wito kwa Kamati ya Usalama na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru kuendeleza ushirikiano waliompatia wakati wa uongozi wake, akieleza kuwa mafanikio aliyoyapata ni matokeo ya mshikamano huo.
“Kwa hakika nawapongeza kwa ushirikiano mliouonesha kipindi chote nilichokuwa nanyi. Ombi langu ni muendeleze ushirikiano huu kwa Mhe. Denis Masanja, kwa kuwa maendeleo ya Wilaya ya Tunduru yanategemea mshikamano miongoni mwetu,” alisema Mhe. Chacha kwa uchangamfu.
Kwa upande wake, Mhe. Denis Masanja alimpongeza mtangulizi wake kwa kazi nzuri aliyoifanya na kuahidi kuendeleza jitihada zote alizoanzisha.
Alieleza kuwa yuko tayari kushirikiana na kila mdau wa maendeleo kwa lengo la kuijenga Tunduru mpya yenye mafanikio makubwa.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.