SERIKALI mkoani Ruvuma imeeleza kuwa Chuo kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA kinatarajia kufungua matawi ya vyuo vikuu katika maeneo ya Madaba,Tunduru na Nyasa mkoani Ruvuma.Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme Akizungumza na wazee na viongozi wa dini katika Ikulu Ndogo ‘mjini Songea amesema chuo kikuu cha SUA tawi la Tunduru kinatarajia kuanza kuchukua wanachuo mwaka huu.
Mkuu wa Mkoa ameongeza kuwa serikali pia imeomba kufungua tawi la chuo kikuu cha Mzumbe mjini Songea na kuongeza kuwa chuo kikuu cha AJUCO Songea kinaweza kufunguliwa na serikali wakati wowote kitakapotimiza vigezo na masharti. TAZAMA HABARI KWA KINA HAPA https://www.youtube.com/watch?v=oZERN6smAS0
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.