WAKALA wa Barabara nchini(TANROADS)mkoa wa Ruvuma,imewatoa hofu watumiaji wa barabara kuu ya Songea-Mangaka kwamba daraja la mto Muhuwesi wilayani Tunduru ambalo lilipata athari ya moja ya sehemu yake kusogea pembeni kwa sasa liko salama.
Hayo yamesemwa na Meneja wa TANROADS mkoani hapa Mhandisi Saleh Juma, baada ya kukagua kazi ya marekebisho ya daraja hilo linalounganisha mkoa wa Ruvuma na mikoa jirani ya Lindi,Mtwara Pwani na Dar es slaam.
Amesema ,TANROADS kwa kumtumia mkandarasi imefanya kazi ya kurudisha sehemu ya kipande kilichotoka sehemu yake na hata maji yalivyopita juu kwa mara ya pili hayakuathiri miundombinu ya daraja hilo muhimu kwa uchumi wa mikoa ya kusini na nchi kwa ujumla.
Msimamizi wa kitengo cha matengenezo TANROADS mkoa wa Ruvuma Mhandisi Roman Mbukwini amesema ,kwa sasa kazi inayofanyika ni kuimarisha baadhi ya sehemu ya barabara ambazo zimeathirika na maji kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha kwa wingi wilayani Tunduru .
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.