mkuu wa Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma Mheshimiwa Aziza Mangosongo ametoa majeneza matatu na kushiriki maziko ya wanafunzi watatu wa shule za Msingi Kindimba chini na Mapendo ambao wamepoteza maisha baada ya kupigwa na radi.
Mangosongo amewataja wanafunzi waliopoteza maisha baada ya kupigwa na radi kutoka shule ya msingi Kindimbachini kuwa ni Maria Hyera mwenye umri wa miaka kumi ,Alfons Hyera miaka minane Deus Kayombo miaka minane kutoka shule ya msingi Mapendano.
Mkuu wa Wilaya pia ametoa rambirambi na kutoa pole kwa majeruhi 11 ambao wanaendelea kupata matibabu katika kituo cha Afya Kindimbachini.
Ili kuhakikisha afya za majeruhi hao zinaimarika Mangosongo amemuagiza Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Kindimbachini kuhakikisha huduma za afya zinatolewa bure.
Akitoa salamu za pole Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Andrew Mbunda amemhakikishia Mkuu wa Wilaya kuwa huduma za afya zitatolewa kwa ubora kama alivyoagiza.
Naye Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Kindimbachini Dkt. Salum Bundala amesema katika tukio hilo wanafunzi watatu wamepoteza maisha, na wanafunzi 20 walijeruhiwa na kufikishwa kituoni hapo kwa ajili ya kupatiwa matibabu ambapo kati yao 9 wameruhusiwa na 11 wanaendelea na matibabu na hali zao zinaimarika.
Akielezea tukio hilo Mwalimu Mkuu wa Shule ya msingi Mapendano Danstan Hyera amebainisha kuwa majira ya saa tisa alasiri radi ilipiga na wanafunzi 23 kati yao 20 walijeruhiwa na wanafunzi watatu walipoteza maisha.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.