Mkuu wa Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma Mheshimiwa Aziza Mangosongo ametoa rai kwa wakulima kulima mazao mengine ya biashara badala ya kutegemea zao la Kahawa peke yake.
Mangosongo ametoa rai hiyo ofisini kwake mjini Mbinga, kwenye mkutano na wakulima pamoja na wadau wa zao la parachichi.
Mkuu huyo wa Wilaya ya Mbinga amewasisitizia wakulima wa kahawa kulima mazao mchanganyiko ili kuwawezesha kupanua wigo wa mapato yao.
“Bei ya kahawa inaposhuka, zao mbadala kama parachichi linaweza kuwa msaada kwako na hivyo kukufanya usitetereke kiuchumi,” alisisitiza Mangosongo na kuongeza kuwa zao la parachichi licha ya kuwa chanzo cha mapato ni rafiki wa mazingira’’,alisema Mangosongo.
Mtaalam wa kilimo katika zao la Parachichin Frank Nyoni amesema kitaalamu parachichi ni tunda lenye virutubisho muhimu sana vinavyohitajika katika mwili wa binadamu na linaongeza kipato kwa familia na Taifa.
Amelitaja soko la parachichi hivi sasa limekuwa sana kutokana na kupeleka zao hilo nje ya nchi Pamoja na usindikaji wa bidhaa zinazotokana na parachichi ambapo hivi sasa bei ya tunda moja la parachichi sokoni inaanzia shilingi 500 hadi 1500
Nchini Tanzania parachichi hulimwa zaidi katika mikoa ya Iringa, Ruvuma,Njombe,Mbeya,Katavi,Rukwa,Morogoro na Kilimanjaro.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.