MKUU wa wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma Julius Mtatiro,ametoa siku kumi na nne(14)kuanzia jana kwa Wakala wa Usambazaji maji vijijini(RUWASA)wilayani humo kwenda kata ya Nampungu ili kufanya tathimini katika eneo la Mto Nampungu kwa ajili ya kuongeza wigo wa upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama kwa wakazi wa kata hiyo.
Mtatiro ametoa agizo hilo jana,akiwa katika ziara yake ya kuzungumza na wananchi,kukagua na kuhimiza shughuli za maendeleo zinazotekelezwa na Serikali kwa kushirikiana na wananchi wa vijiji mbalimbali wilayani humo.
Alisema,wananchi wa kata hiyo wanakabiliwa na kero kubwa ya huduma ya maji safi na salama licha ya kuwa na chanzo kikubwa na cha uhakika ambacho ni mto maarufu wa Nampungu unaotiririsha maji majira yote ya mwaka.
Ameitaka Ruwasa kuhakikisha wanamaliza kero hiyo ili wananchi wapate nafasi ya kufanya shughuli zao za kujiletea maendeleo,badala ya kutumia muda mwingi kwenda kutafuta maji kwa ajili ya matumizi yao ya kila siku.
Aidha,amewataka wananchi wa wilaya ya Tunduru kuendelea kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan na Serikali yake ya awamu ya sita kwani katika kipindi cha mwaka mmoja wilaya hiyo imepokea zaidi ya Sh.bilioni 23 kwa ajili ya kutekeleza shughuli za maendeleo.
Pia katika ziara hiyo, Mtatiro amekagua barabara ya urefu wa km 27 inayojengwa kwa kiwango cha Changarawe kutoka Nandembo hadi Nampungu ambayo imemaliza changamoto ya mawasiliano kwa wakazi wa kata hizo mbili.
Mtatiro amempongeza Meneja wa Tarura wilayani humo Mhandisi Silvanus Ngonyani, kwa kazi na matumizi mazuri ya fedha za Serikali ambazo zimewezesha kujenga miradi mikubwa kuliko bajeti iliyoletwa wilayani humo.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.