Mkuu wa wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma Mheshimiwa Ngollo Malenya wa kwanza kulia amefanya ziara ya kukagua miradi ya ujenzi wa madarasa ,vyoo, chumba Cha kujifungulia na Kutoa maagizo mbalimbali.
Malenya amekagua chumba Cha kujifungulia katika zahanati ya Kijiji Cha Lumecha ,ujenzi wa madarasa katika Shule shikizi ya Lumecha ,shule ya Sekondari Namabengo, Shule mpya ya Suruti pamoja na Shule ya msingi Namwaya.
Katika ukaguzi huo Mkuu wa wilaya amesisitiza uwajibikaji wa kamati katika kusimamia ujenzi Kwa kuhakikisha mafundi wanalipwa stahili zao , vifaa vinanunuliwa Kwa wakati na mafundi wafanye kazi ya ujenzi na kukamilisha miradi Kwa wakati .
i..
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.