Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma wametakiwa Kuimarisha Ulinzi katika Maeneo ya Hifadhi ili kulinda rasilimali za Misitu.
Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo Mheshimiwa Ngollo Malenya baada ya kufanya Ukaguzi wa Hifadhi ya msitu wa Matogoro B upande kijiji cha Luhimbalilo katika kata ya Mputa.
Malenya amewataka Wananchi katika kijiji hicho Kuondoka haraka katika Maeneo ya hifadhi na kuendelea kulinda na kutunza mazingira.
Amewaonya viongozi wa vijiji na Kata kujiepusha na utoaji wa vibali vya kuwaruhusu Wananchi kuingia na kufanya Shughuli mbalimbali za Kibinadamu ikiwemo kilimo na ufugaji katika Hifadhi hiyo.
"Sisi kama Kamati ya Ulinzi na Usalama tutaendelea kufuatilia na kuhakikisha kwamba Uharibifu haufanyiki kwa ajili ya Maslahi ya Wana Namtumbo na Mkoa wa Ruvuma kwa Ujumla’’,alisisitiza Malenya.
Meneja Uhifadhi wa Misitu Tanzania katika Wilaya ya Namtumbo Vicent Walter ameahidi kutekeleza maagizo ya Mkuu wa Wilaya ili maelekezo kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ili kulinda hifadhi hiyo ya Matogoro B,yenye ukubwa wa hekta 32,900 iliyopo katika Kata ya Hanga wilayani Namtumbo.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.