Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma Mheshimiwa Ngollo Malenya amewapongeza wakulima kwa kuongeza uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara.
Amesema katika wilaya ya Namtumbo Kwa msimu wa 2022/2023 Wakulima Walilima hekta 42,354 zilizozalisha tani 152,995 za mahindi.
Ameongeza kuwa katika msimu wa mwaka 2023/2024 Wakulima wilayani humo wamezalisha hekta 50,536 zinazotarajia kuzalisha tani 182,550 za mahindi.
Mkuu wa wilaya ya Namtumbo ili kuwatia moyo wakulima amefanya ziara ya siku Moja kutembelea mashamba ya wakulima na kuzungumza nao wakiwa katika mashamba yao.
Juma Zuberi ni Mkulima wa kijiji cha Namabengo amesema mafanikio ya wakulima yametokana na upatikanaji wa pembejeo hasa mbolea ya ruzuku
Mkoa wa Ruvuma umekuwa ghala la Taifa la chakula kwa kuongoza katika uzalishaji wa mazao ya nafaka nchini.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.