Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Mheshimiwa Filberto Sanga amewataka na kuwahimiza Madiwani wa Halmashauri wa Wilaya hiyo pamoja na wataalamu wakilimo kuendelea na zoezi utoaji elimu kwa wakulima kuhusu zeozi la uandikishwaji wa pembejeo za kilimo
Akizungumza kwenye kikao cha Baraza la madiwani la Halmashauri hiyo wakati wa kujadili taarifa ya robo nne ya (April-June 2023) kilichofanyika hivi karibuni kwenye ukumbi wa Halmashauri Kilosa Mbambabay.
Sanga amesema kuelekea msimu ujao wa kilimo lazima wakulima washirikishwe katika uandikishwaji wa kupata pembejeo lengo ni kupata takwimu halisi ya mahitaji ya pembejeo kwa wakulima
“Niwaombe sana viongozi wezangu tushirikiane kuhakikisha kwamba kila kijiji na kata tunakuwa na hesabu sahihi ya wakulima na mahitaji sahihi ya pembejeo ili tunapoomba ngazi ya mkoa tuweze kupata kulingana na idadi ya wakulima na idadi ya maeneo tutakayo lima”
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.