Chuo cha Ufundi Stadi VETA wilaya ya Nyasa kimefanya Mahafali yake ya kwanza mahafali yaliyofanyika katika Viwanja vya Chuo hicho na Mgeni Rasmi katika Mahafali hayo alikuwa ni Mkuu Wa Wilaya ya Nyasa Mhe. Peres Magiri .
Mhe. Magiri amewataka wananchi wa Wilaya ya Nyasa kusoma chuo cha VETA Nyasa kwa lengo la kupata ujuzi utakaowasaidia kujiajiri, na kuongeza kipato kwa mtu mmoja, kaya na Taifa kwa ujumla. Uwezo wa Chuo hiki ni kuchukua wanafuznzi zaidi ya 160, lakini mpaka sasa chuo hiki kinadahili wanafunzi 80 hivyo basi tunatakaiwa kutumia fursa hii kupata ujuzi.
Mhe Magiri ameongeza kuwa Elimu ya Ufundi haina mipaka ya umri cheo hivyo basi wananchi wote tunatakiwa kupata ujuzi ambao ambao utatusaidia kuongeza kipato cha ziada na kuboresha maisha yetu,
“ Nimejipa ubalozi wa kukitangaza Chuo cha Ufundi Stadi VETA Nyasa, Sijaridhika na jinsi wananyasa tunavyokitumia Chuo hiki kwa kuwa bado tunakuwa na nafasi nyingi za kusoma lakini hatutaki kuleta vijana wetu’’,alisema.
Amewasihi wahitimu kwenda vijijini na kutumia ujuzi wao kwa kuanzisha vikundi kwa kufanya shughuli walizosomea na Serikali itawaunga mkono kwa kuwakopesha Asilimia kumi ya mapato, badala ya kwenda mijini kupoteza muda.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.