Mkuu wa Wilaya ya Nyasa, Mhe. Peres Magiri, amezindua rasmi kampeni ya upandaji miti katika Kata ya Luhangarasi, iliyofanyika kwenye shamba la Shule ya Msingi Luhangarasi wilayani Nyasa. Kampeni hiyo, iliyoandaliwa kwa kushirikiana na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), inalenga kuunga mkono juhudi za Serikali katika kutunza mazingira.
Katika uzinduzi huo, miti ilipandwa katika eneo la shule na kugawiwa kwa wananchi ili wapande kwenye maeneo yao. Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya, Afisa Tawala wa Wilaya ya Nyasa, Bw. Benedicto Nsindagi, amewasisitiza wananchi kupanda miti na kuitunza ili kuimarisha mazingira na kuona matokeo chanya ya juhudi hizo.
Bw. Nsindagi pia amewahimiza wananchi kupanda miti ya matunda kwa ajili ya lishe bora na kupunguza changamoto ya lishe duni. Aidha, aliwataka kushirikiana na kuhimizana kupanda miti zaidi hasa katika kipindi cha masika ili kufanikisha kampeni hiyo kuwa endelevu.
Kwa upande wake, Meneja wa TFS wilayani Nyasa, Bw. Elisha John, amesema wakala huo umetenga miche 30,000 kwa ajili ya wananchi.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.