Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma Joseph Rwiza amewataka wanafunzi wote kuzingatia masomo na kutambua jitihada zinazofanywa na wazazi wao za kuhakikisha wanapata elimu bora.
Amewataka wanafunzi hao kutambua azma ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ya kuimarisha na kuboresha sekta ya elimu nchini.
Rwiza ametoa wito huo alipozungumza na wanafunzi wa shule za Sekondari Ruanda na Litumbandyosi katika ziara yake ya kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
" Nafasi hii mlioipata itumieni vizuri wazazi wanataka mpate elimu bora lakini pia Rais wetu amewekeza fedha nyingi ili tujifunze katika mazingira rafiki" Amebainisha Rwiza
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.