Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Namtumbo, mkoani Ruvuma Philemon Mwita Magesa, ameagiza ujenzi na usimamizi wa miradi mbalimbali kufanyika kwa saa 24 ili kuhakikisha inakamilika kwa wakati.
Miongoni mwa miradi hiyo ni ujenzi wa mapitio (walkways) katika Hospitali ya Wilaya ya Namtumbo.
Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo, Dr. John Chacha Nyagana, amesema mfumo wa kazi kwa saa 24 utaongeza ufanisi na kuharakisha utekelezaji wa mradi hii
. “Mkandarasi na mafundi wanaendelea na kazi bila kusimama, jambo linalowezesha kukamilika kwa wakati,” alisema Dr.Nyagana.
Dr Nyagana amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, kwa kutenga fedha nyingi kuboresha sekta ya afya, ikiwemo ujenzi wa hospitali na miundombinu yake.
Ujenzi wa mapitio hayo unatarajiwa kuboresha huduma kwa wagonjwa na wahudumu wa afya, huku serikali ikiendelea kusisitiza utekelezaji wa miradi kwa wakati na kwa viwango vinavyotakiwa.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.