Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo, mkoani Ruvuma Philemon Mwita Magesa, amewataka wakuu wa idara na vitengo kusimamia miradi yote inayoendelea kutekelezwa katika halmashauri hiyo kwa muda wa usiku na mchana ili kuhakikisha inakamilika kwa wakati.
Akizungumza katika kikao kazi cha Timu ya Wataalamu wa Halmashauri (CMT) ofisi yake, Magesa alisisitiza umuhimu wa kuhakikisha mafundi wanaosimamia miradi wanakamilisha kazi zao kwa viwango vilivyopangwa na serikali.
“Miradi yote inayotekelezwa katika Halmashauri yetu ya Namtumbo lazima ikamilike kwa wakati. Hakikisheni kazi inafanyika usiku na mchana, mafundi wasimamiwe ipasavyo, na kazi zifanyike kwa viwango vya ubora kama ilivyopangwa,” alisema Magesa.
Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo imekuwa ikitekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo, na hatua hiyo inalenga kuboresha ufanisi na kukidhi matarajio ya serikali na wananchi.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.