Mradi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo, mkoani Ruvuma, umekamilika kwa mafanikio makubwa kutokana na jitihada za Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Philemon Magesa.
Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ilitoa zaidi ya shilingi bilioni 4.3 kwa ajili ya kujenga shule hiyo maalum ya wasichana, itakayowahudumia wanafunzi wa kidato cha kwanza hadi cha sita.
Ili kuhakikisha mradi huo unakamilika kwa ubora na kwa wakati, Magesa aliweka mikakati madhubuti ya usimamizi, ikiwemo kubadilishana zamu za kazi kwa mafundi na kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kwa ufanisi kulingana na viwango vilivyowekwa na Serikali.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.