Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma Philemon Magesa ameunda timu itakayohusika na Ufuatiliaji na kufanya tathmini ya miradi mbalimbali kabla ya Kufanya Malipo kwa Mkandarasi, Fundi au Mzabuni.
Akizungumza Katika kikao kazi na watendaji kutoka katika kata 21 za Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo kilichofanyika mjini Namtumbo,Magesa amewataka watendaji kata Kuwa makini katika usimamiaji na ufuatiliaji wa miradi katika kata zao.
Amesema uwepo wa timu hiyo itasaidia kufanya Malipo kwa Mkandarasi, Fundi au Mzabuni aliye kidhi vigezo vya mahitaji ya Halmashauri hiyo na kwamba timu itahakikisha miradi inatekelezwa kwa viwango.
Amesema timu hiyo pia itaangalia vifaa na mahitaji yanayonunuliwa kama yapo katika mpango wa mradi huo ili Mkandarasi, Fundi au Mzabuni aweze kulipwa Stahiki kihalali.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.