MKURUGENZI Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma Khalid Khalif amewataka watumishi wa Umma kuongeza kasi ya ukusanyaji mapato ya ndani ya Halmashauri na kuziba mianya ya utoroshaji mapato,
Akizungumza katika kikao cha Baraza la Wafanyakazi kilichofanyika Ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Nyasa Khalid amesema ili Halmashauri iweze kuwalipa Stahiki wafanyakazi, inategemea kukusanya mapato ya ndani , hivyo ni wajibu wa kila mtumishi kuhakikisha mapato ya ndani yanakusanywa
“Suala la kukusanya mapato ya ndani ni la kwetu sote watumishi, na hakuna anayependa mtumishi asilipwe stahiki zake, kila mtumishi popote alipo ahakikishe anakusnya mapato na kuziba mianya ya kutorosha mapato”,alisema.
Hata hivyo Khalif amewapongeza watendaji wa Kata na Vijiji kwa kazi nzuri ya kukusanya mapato ya ndani kwa kuwa mpaka sasa wamekusanya shilingi bilioni 1.4 sawa na asilimia 92 ya mapato ya ndani.
Amewataka kuongeza bidii ili kufikia malengo ya kukusanya shilingi bilioni 2.4 katika mwaka wa fedha wa 2024/2025.
Baraza la wafanyakazi wa Halmashauri ya Nyasa limempongeza Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Nyasa Bw. Khalid Khalif kwa mikakati ya kulipa Stahiki za wafanyakazi, na kupandisha kiwango cha kulipa watumishi hodari wa mwaka kutoka shilingi 200,000 hadi 500,000.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.