Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya mkoani Ruvuma Songea Bi. Elizabeth Mathias Gumbo amewataka mafundi kuongeza kasi ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ili iweze kukamilika kwa wakati .
Gumbo ametoa maagizo hayo baada ya kukagua ujenzi Miradi saba inayotekelezwa katika Halmashauri hiyo.
“ Tupo nyuma ya muda, tunayo pesa ya kutosha hivyo kwa wale wote wanaosimamia miradi hakikisheni mnashinda site na kusimamia mafundi muda wote”, alisema Gumbo.
Miradi iliyokaguliwa na Mkurugenzi huyo ni pamoja na Shule ya Sekondari Maposeni ambapo alikagua Ujenzi wa jengo la utawala lililotengewa Zaidi ya shilingi milioni 74, Ujenzi wa Madarasa 17 yenye thamani ya Zaidi ya Shilingi 408 na Matundu 25 ya vyoo yenye thamani ya Zaidi ya 44.
Miradi mingine aliyaikagua ni madarasa 10 katika Shule ya Sekondari Jenista Mhagama, alipita na kukagua ujenzi wa Madarasa kumi yenye ya shilingi milioni 240 na Matundu ya Vyoo 19 yenye thamani ya Shilingi milioni 33.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.