Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini na Waziri wa Sheria na Katiba, Mhe. Dkt Damas Ndumbaro, amezindua jengo lenye vyumba viwili vya madarasa pamoja na ofisi ya Mkuu wa Shule katika Shule ya Msingi Majimaji.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Dkt Ndumbaro alisema ujenzi huo umefanikishwa kupitia Taasisi ya SOMI, ambayo iliomba msaada wa kifedha kutoka Ubalozi wa Ujerumani kwa ajili ya ukarabati wa majengo ya shule hiyo.
Jumla ya shilingi milioni 52 zilitolewa kufanikisha mradi huo.
Naye Mwenyekiti wa CCM Songea Mjini, Ndugu Mwinyi Msolomi, amepongeza juhudi za Mbunge huyo katika sekta ya elimu, akiahidi kuwa Chama cha Mapinduzi kitaendelea kushirikiana naye na viongozi wengine katika kuimarisha maendeleo ya wananchi.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.