MPANGO wa Elimu bila malipo umeongeza uandikishaji wa Elimu ya Awali katika Halmashauri za Mkoa wa Ruvuma kutoka wanafunzi 42,140 mwaka 2022 hadi kufikia wanafunzi 44,853 mwaka 2023.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas amesema Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassani imeendeleza mpango wa elimu bila malipo katika Mkoa wa Ruvuma ili kuboresha elimu kuanzia Elimu ya awali.
“Elimu ya Awali ni hatua muhimu ya Maandalizi katika mzunguko wa elimu, Serikali ya Tanzania imeijumuisha elimu hii kwenye mfumo rasmi wa elimu na kuagiza kila shule ya msingi iwe na darasa la elimu ya awali litakaloandikisha watoto wenye umri wa miaka mitano hadi sita’’,alisisitiza RC Thomas.
Ameongeza kuwa Mkoa wa Ruvuma pia umepata mafanikio katika uandikishaji wa Watoto wa darasa la kwanza kutoka wanafunzi 45,243 mwaka 2022 hadi kufikia idadi ya wanafunzi 45,394 mwaka 2023.
Sera ya Elimu na Mafunzo (ETP) ya mwaka 1995, inakusudiwa kuhimiza maendeleo ya haiba ya mwanafunzi sifa za kimwili, kiakili, kimaadili na uwezo.
Mkoa wa Ruvuma una jumla ya wanafunzi 387,526 wanaosoma kuanzia darasa la Awali hadi la saba hadi kufikia Machi, 2023.kati yao wavulana 194,666 na wasichana 192,860.
Imeandikwa na Farida Baruti
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma
Oktoba 13,2023
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.