Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango amewaasa watanzania kutumia fursa ya mikutano ya kisiasa kufanya siasa za kistaarabu ili kuendeleza amani na utulivu uliopo nchini.
Makamu wa Rais amesema hayo wakati akizungumza kwa nyakati tofauti na wananchi wa vijiji vya Lilondo Halmashauri ya Madaba wilaya ya Songea na wananchi wa kijiji cha Mlilayoyo Halmashauri ya Namtumbo mkoani Ruvuma ambako ameanza ziara ya kikazi ya siku tano.
Amesema si vema kutumia lugha zisizo na staha katika kufanya siasa kwa sababu zinaweza kusababisha uvunjifu wa hali ya amani na utulivu.
Katika hatuia nyingine ya maendelea Makamu wa Rais amesema katika mwaka huu wa fedha serikali itajenga upya barabara ya lami yenye urefu wa kilometa 98 kipinde cha Litukila - Songea kilom ili kukabiliana na changamoto za miundombinu ya barabara ya Songea hadi Makambako ambaye imechakaa na inatakiwa kujengwa upya.
Pia ameigiza wizara ya maji kupeleka shilingi milioni 150 katika Kijiji cha Lilondo zitakazowezesha usambazaji wa miundombinu ya maji ili kutoa huduma kwa wananchi wa eneo hilo.
Akiwa katika Kijiji cha Mlilayoyo, Makamu wa Rais amekemea uingizwaji kwa wingi wa mifugo hususani ng’ombe hali inayochochea katika uharibifu wa mazingira.
Ameuagiza uongozi wa Mkoa wa Ruvuma kufanya tathimini ya mifugo iliopo na uwezo wa mkoa huo katika kupokea ng’ombe hizo.
.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.