Naibu katibu mkuu wa Wizara ya Maliasili na utalii Dkt.Aloyce Nzuki amesema serikali inatarajia kurejesha nchini fuvu la jemedari wa kabila la wangoni Nduna Songea Mbano pamoja na mafuvu 200 ya mashujaa yaliyopo nchini Ujerumani na kwamba mafuvu hayo yafanyiwa maziko upya na kwa heshima wanayostahili. mashujaa hao ambao walikubali kumwaga damu kwa ajili ya kujikomboa dhidi ya wakoloni.
Dkt.Nzuki alikuwa anatoa salama za Wizara ya Maliasili na Utalii katika kumbukizi ya miaka 113 ya mashujaa wa vita ya Majimaji kwenye viwanja wa Makumbushoi ya Taifa ya Majimaji mjini Songea ambako mashujaa 67 walizikwa baada ya kunyongwa na wajerumani mwaka 1906.TAZAMA HABARI KWA KINA HAPA https://www.youtube.com/watch?v=nLvF4qzzdnk&t=89s
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.