MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Generali Wilbert Ibuge amesema amedhamiria kuimarisha sekta ya nishati kwa kuhakikisha Mkoa unazalisha umeme wa kutosha.
RC Ibuge amesema hali ya upatikanaji wa umeme baada ya kuunganishwa na gridi ya Taifa ni ya kuridhisha katika wilaya zote za Mkoa wa Ruvuma.
Amesema kuwa katika Mradi wa REA awamu ya tatu mzunguko wa kwanza fedha kiasi cha Zaidi ya Bilioni 43 zimepokelewa kwaajili ya kupeleka umeme kwenye vijiji 177, pia Mradi wa REA awamu ya tatu mzunguko wa pili fedha Zaidi ya Bilioni 71 zimetengwa kupeleka umeme kwenye vijiji 235.
‘’Hatua ya utekelezaji wa Mradi umefika asilimia 7 wakandarasi waliopewa kazi wameshamaliza kazi ya upimaji na kazi ya kuanza kuleta nguzo imeshaanza Mradi huu unategemewa kumalizika mwezi Februari, 2023’’, amesema RC Ibuge.
Hata hivyo amesema kutokana na utekelezaji wa Mradi wa Gridi ya Taifa Ruvuma imefanikiwa kupunguza gharama za uendeshaji wa TANESCO baada ya kuzima mitambo inayotumia mafuta ambapo fedha hizo zitatumika kwenye uimarishaji wa huduma kwa wateja na miundo mbinu. Pia Mradi umetoa fursa za ajira,umeboresha huduma za afya na elimu pamoja na kuboresha mawasiliano.
Imeandaliwa na Bahati Nyoni
Kutoka Ofisi ya Habari Mkoa wa Ruvuma
Februari 09,2022.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.