Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Mbinga mkoani Ruvuma Dkt. Kung’e Nyamuryekung’e amesisitiza umuhimu wa kuongeza idadi ya shule zinazotumia unga ulioongezwa virutubishi ili kukabiliana na changamoto ya utapiamlo na udumavu.
Akizungumza kwenye kikao cha Kamati ya Lishe ya Halmashauri hiyo, Dkt. Nyamuryekung’e amesema matumizi ya unga wa virutubishi huo katika shule hauridhishi.
Kutokana na hali hiyo amewaagiza maafisa elimu na maafisa lishe kushirikiana katika utoaji wa elimu kuhusu umuhimu wa kutumia unga ulioongezwa virutubishi.
“Wakazi wa Halmashauri ya Mji wa Mbinga wapewe elimu kuhusu uwepo wa mashine zinazoongeza virutubishi kwenye unga na umuhimu wa matumizi ya unga huo,” alisisitiza Dkt. Nyamuryekung’e.
Kwa upande wake Afisa Lishe wa Halmashauri ya Mji wa Mbinga Gloria Maya amesema watashirikiana na Idara ya Viwanda na Biashara ya Halmashauri pamoja na watendaji wa kata kuhakikisha wanafunzi na jamii kwa ujumla wanatumia unga ulioongezwa virutubishi.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.