Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma imevuka lengo katika ukusanyaji wa mapato kwa kukusanya Zaidi ya shilingi bilioni 7.76 kutoka katika vyanzo mbalimbali vya mapato ya ndani katika mwaka wa fedha wa 2023/2024.
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Kitengo cha Fedha na Uhasibu CPA. Samwel Marwa katika kikao maalum cha Baraza la Madiwani kujadili taarifa za hesabu za Halmashauri kilichofanyika katika Halmashauri hiyo.
Amesema, katika mwaka huo wa fedha Halmashauri hiyo iliidhinishiwa kukusanya shilingi 6,300,000,000 ambapo hadi kufikia Februari kiasi cha shilingi 5,050,776,560.11 kilikusanywa sawa na asilimia 80 ya makusanyo.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.