Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea, Mwl. Neema Maghembe, amekabidhi vitabu vya kiada kwa Walimu Wakuu wa Shule za Msingi waliopo Halmashauri ya Wilaya ya Songea kwa lengo la Kuhimiza matumizi ya Mtaala ulioboreshwa, unaowahusu wanafunzi wa Elimu ya Awali, Darasa la kwanza na darasa la tatu.
Halmashauri ya Wilaya ya Songea, imepokea vitabu vya Kiada vya Elimu ya Awali na Msingi Darasa la I, III na Mihtasari vya mtaala ulioboreshwa vyenye thamani ya shillingi 12,930,529/= kutoka Taasisi ya Elimu Tanzania ( TET) ambapo Mkurugenzi Mtendaji amevisambaza kwa Shule zote za Msingi na kusisitiza matumizi ya vitabu hivyo.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.