Mkuu wa mkoa wa Ruvuma, Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge ameipongeza Halmashauri ya wilaya ya Tunduru kwa kuvuka lengo kwa kukusanya mapato ya ndani zaidi ya Bilioni tatu ambapo makadirio yalikuwa bilioni bilioni 2.5 n kwa mwaka.
Aidha Mkuu wa mkoa wa Ruvuma amempongeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru Ndugu Gasper Zahoro Balyomi kwa kuweza kulipa staiki zote za madiwani kwa wakati adi sasa hakuna diwani hata mmoja anaedai staiki zake katika Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru pia Mkuu wa mkoa wa Ruvuma ameipongeza Halmashauri kwa kutoa kiasi cha Milioni miambili ishilini na nne ni 10% ya Wanawake, Vijana na walemavu.Pia Mheshimiwa Mkuu wa mkoa wa Ruvuma amewataka Wakuu wa Idara na Vitengo wa Halmashauri ya wilaya ya Tunduru kuacha kujibu hoja za CAG kwa mazoea kwani hali hiyo ya kujibu hoja za CAG kwa Mazoea ndiyo iliyoa pelekea kupata hati yenye Mashaka aidha Mkuu wa mkoa alisema kuwa kwa miaka mitano mfululizo kuanzia mwaka 2014-2015 mpaka 2018-2019 Halmashauri ya wilaya ya Tunduru imepata hati safi sasa kwa mwaka 2019 – 2020 kwa Halmashauri ya wilaya ya Tunduru kupata Hati yenye shaka kwa hali hii Wakuu wa Idara wanatakiwa kuacha kujibu hoja kwa mazoea ili Halmashauri ya Tunduru iweze kurejea kupata hati safi kama kawaida yake.
Mkuu wa mkoa amewataka Waheshimiwa madiwani wanapo kuwepo katika maeneo yao ya kiutwala washirikiane na uongozi wa vijiji vyao kuhakikisha hakuna raia yeyote kutoka Nchi jirani ya Msumbiji ana vuka mpaka kuingia Tanzania kwani Hali ya kiusalama kwa majirani zetu msumbiji sio zuri hivyo viongozi na wananchi wanaoishi vijiji vya mpakani ndio walinzi namba moja katika kuhakikisha Wahamiaji haramu hawaingii katika Nchi yetu ya Tanzania.
Imeandikwa na Afisa Habari wilaya ya Tunduru
Juni 15,2021
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.