MKOA wa Ruvuma umeweka mikakati ya kuzuia migogoro ya wakulima na wafugaji na watumiaji wengine wa ardhi.
Afisa Mifugo wa Mkoa wa Ruvuma Nelson William amesema Halmashauri za Wilaya za Mkoa wa Ruvuma kwa kushirikiana na chama cha wafugaji (CCWT) waone umuhimu wa kufanya Sensa ya Mifugo.
Amesema mikakati hiyo ikiwemo kutambua wafugaji na mifugo iliyopo katika kila kijiji ili kujua takwimu sahihi ya mifugo katika upangaji wa mipango ya ardhi,miundombinu ya mifugo na huduma za jamii.
Hata hivyo amesema Halmashauri za Wilaya za Mkoa wa Ruvuma zione uwezekano wa kufanya utaratibu wa kuwatengea wafugaji eneo la kuchungia katika vijiji vilivyoainishwa kwaajili ya ufugaji na kuwekewa mipaka ya kudumu.
“Kila Halmashauri ione umuhimu wa kuwaelimisha na kuwahamasisha wafugaji juu ya umuhimu wa utoaji wa takwimu sahihi za mifugo”.
Wiliam amesema Wafugaji na wakulima walio katika maeneo yasiyo rasmi mfano hifadhi ya misitu ya Muhuwesi,Sasawala na Ushoroba wa Kilimasera waondoke kwa hiari waende katika maeneo yatakayoruhusiwa kuchungia.
“Halmashauri zione uwezekano wa kukamilisha mipango ya matumizi bora ya ardhi kwa vijijivyenye wafugaji,wahamiaji wakulima wazawa na watumiaji wengine”.
Amesema Halmashauri za Mkoa zione umuhimu wa kushirikiana na asasi zingine kwa mfano MVIWATA,RUCODIA,PASS,pamoja na wadau wenginewa maendeleo na makundi ya wafugaji ,chama cha wafugaji katika zoezi la uandaaji wa mipango ya matumizi bora ya ardhi.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma
Agosti 30,202.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.