Hospitali ya Wilaya ya Namtumbo, mkoani Ruvuma ambayo ilianza kutoa huduma zake mwaka 2014 na kuanza huduma za upasuaji mwaka 2022, inaendelea kuwa kituo muhimu cha huduma za afya kwa wakazi wa wilaya hiyo.
Kulingana na taarifa ya Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo, Dr.Aron Hyera hadi sasa , hospitali hiyo inajivunia kuwa na jumla ya majengo 16 yaliyojengwa kwa gharama ya zaidi ya shilingi bilioni tatu
“Majengo hayo yamekamilika na yanatumika, yakiwemo jengo la maabara, jengo la huduma za baba, mama na mtoto, jengo la macho, pamoja na jengo la afya ya kinywa”,alisema.
Amezitaja huduma zinazotolewa hospitalini hiyo kuwa ni pamoja na matibabu ya wagonjwa wa nje, huduma za maabara kwa vipimo mbalimbali, radiolojia, na kulaza wagonjwa wa aina mbalimbali, ikiwemo wanawake wanaojifungua na wanaohitaji upasuaji wa uzazi.
Aidha, hospitali hiyo inatoa huduma za kulaza wagonjwa wa kike, wa kiume, na watoto.
Hata hivyo amesema hivi karibuni, hospitali hiyo ilipokea kiasi cha shilingi milioni 575 kwa ajili ya kuboresha huduma zake. Kati ya fedha hizo, milioni 300 zimetengwa kwa ununuzi wa vifaa tiba.
Amesema zaidi ya milioni 200,zimetolewa kwa ujenzi wa miundombinu ya maji na ujenzi wa njia za kutembelea (walkways) ambazo zitaunganisha majengo yote ya hospitali hiyo.
Hatua hizi zinatarajiwa kuboresha zaidi huduma zinazotolewa hospitalini hapo na kuimarisha ustawi wa afya ya wakazi wa Wilaya ya Namtumbo.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.