KATIBU Tawala Mkoa wa Ruvuma Ndugu Stephen Ndaki akiwa na Timu ya Menejimenti Mkoa wamekagua mradi wa ujenzi wa Jengo la Wagonjwa wa Dharura (EMD) katika hospitali ya wilaya ya Nyasa ambalo serikali imetoa shilingi milioni 300 kutekeleza mradi huo ambao hadi sasa bado haujakamilika kwa asilimia 100 .
Akizungumza baada ya ukaguzi wa jengo hilo Ndaki amesikitishwa na ucheleweshaji wa mradi huo ambapo amesema kuna changamoto kubwa kwenye umaliziaji wa fremu na ufungaji milango na kwamba kazi ya kuanza kufunga vifaa kwenye jengo la EMD imechelewa ukilinganisha na hospitali nyingine za Tunduru na Madaba ambazo tayari zimefunga vifaa kwenye kwenye majengo hayo.
Amesema kasi ya umaliziaji ni ndogo hivyo ameuagiza uongozi wa Halmashauri hiyo kuongeza kasi ya ukamilishaji na kufanya marekebisho kwenye frame na milango ambapo amewataka kusimamia utekelezaji wa miradi kuanza hatua za awali hadi mwisho ili utekelezaji wake uwe wenye viwango na ubora.
Kwa upande wake Mkuu wa WIlaya ya Nyasa Mheshimiwa Filibetho Sanga amesema kumekuwa na usimamizi mbovu kwenye miradi ya serikali hali inayosababisha miradi kutekelezwa chini ya viwango na miradi mingine kutokamilika kwa wakati
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.