• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

HUDUMA za matibabu ya ubingwa bobezi kutolewa Mwengemshindo Songea

Imewekwa kuanzia tarehe: September 22nd, 2024

Ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, Songea itawezesha upatikanaji wa huduma za ubingwa bobezi ikiwemo huduma za magonjwa ya akina mama na uzazi, magonjwa ya Upasuaji, magonjwa ya Ndani, magonjwa ya Watoto, magoniwa ya Kinywa na Meno, Macho, Masikio, Pua na Koo pamoja na huduma ya Mionzi.

Waziri Mhagama amesema hayo  alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Hospitali hiyo iliyopo katika Kata ya Mwengemshindo, Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma ambapo ameambatana na Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala na Rasilimali watu, Hospitali za Rufaa za Mikoa Bw. Danny Temba, Mkurugenzi wa huduma za Tiba Dkt. Hamadi Nyembea, Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Sera na Mipango Bw. Tumainieli Macha.

“Awali ili mtu apate matibabu haya ilikua lazima aende Muhimbili, na wakati mwengine ilikua lazima aende kutibiwa nje ya nchi, uwezo wetu kwa wananchi wengi ni mdogo, Serikali itakusaidia kumtibu mgonjwa lakini kumuuguza ni garama nyingine, huduma hizo kwa sasa zinapatikana hapa hapa Mwengemshindo ili kuokoa garama za mwananchi kutafuta tiba.” Amesema Waziri Mhagama

Waziri Mhagama amesema jengo hilo limekaa muda mrefu bila kukamilika, hivyo amekabidhi hundi ya fedha kiasi cha Shilingi Milioni 283,467,765.60/= ili apewe mkandarasi aendelee na ujenzi wa Hospitali hiyo ambayo ameelekeza ikamilike katika maeneo ambayo bado hayajakamilika kabla ya mwezi Februari 2025 huduma zianze kutolewa.

Aidha, Waziri Mhagama amesema ndani ya miaka Mitatu ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imefanyika uwekezaji mkubwa kwenye Sekta ya Afya ikiwemo miundombinu ya majengo ambapo ametoa Shilingi Bilioni 3.8 ili kujenga Hospitali hiyo ya Rufaa ya Mkoa wa Songea, ununuzi wa vifaa, vifaa tiba ikiwemo mashine za MRI pamoja na CT-Scan. I

“Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ameagiza kuwekeza mradi wa ujenzi wa Hospitali hii ya Rufaa ili kiu ya wananchi wa Kata ya Mwengemshindo, wananchi wa Songea na wanaruvuma kwa ujumla ili kuhakikisha wanafikiwa na huduma za Afya zenye viwango.” Amesema Waziri Mhagama

Amesema, Serikali kupitia Wizara ya Afya imejipanga kutoa huduma za tiba kwa magonjwa hayo ikiwemo magonjwa yanayohitaji huduma za kibingwa zipatikane kwa bei nafuu na inayowezekana kwa kila mwananchi wa Mwengemshindo na Watanzania kwa ujumla.

Waziri Mhagama amewataka wananchi wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea kuchagua wahudumu wa Afya ngazi ya Jamii watakaosaidia kuibua wagonjwa kwenye maeneo yao ambao katika kila mtaa kutakua na wahudumu Wawili (Wakike na Wakiume).

“Wahudumu hawa wa Afya ngazi ya jamii, watapita katika maeneo yetu kutupima, na kama utagundulika kuwa una tatizo lolote la kiafya watakushauri uende hospitali kwa matibabu zaidi, na huduma hizi zitatolewa bila malipo, zitalipiwa na Serikali.” Amesema Waziri Mhagama.


Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MBINGA-MBAMBABAY : barabara inayojenga utalii kwenye milima ya Kusini

    June 01, 2025
  • PICHA ya Rais Samia yapamba mti wa kihistoria Namtumbo

    June 01, 2025
  • TAIFA lamlilia Songambele Shujaa wa Uhuru aliyeishi karne moja

    June 01, 2025
  • SHAMBA la AVIV Tanzania ni mfano wa kuigwa nchini

    June 01, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.